Effective Microorganisms

EM.1® ni nini?

FEEDPRO EMAX > EM.1® ni nini?

EM.1®
ni nini?

Effective Microorganisms (EM.1®) ni mchanganyiko wa vijidudu vidogo vidogo (visivyoonekana kwa macho ya kawaida) tofauti vinavyopatikana kwa uhalisia na ambavyo vipo katika kundi la vyakula.

Viumbe hawa ni halisia na wanatokana na mazingira tunayoishi na si wa kuzalishwa maabara. EM.1® ni teknolojia inayofanya vijidudu hao kuweza kuishi na kufanya kazi kwenye mazingira yasiyokuwa na hewa ya oksijeni na pia kwenye mazingira yaliyo na hewa ya oksijeni. EM.1® sio kiua wadudu, dawa, mbolea na wala si kemikali ya viwandani. EM.1® huongezwa kwenye maji taka ili kuboresha vijidudu wadodo wadogo waliomo na kuondoa harufu mbaya pia kuchakata uchafu. Pia viumbe hawa husaidia kuozesha taka za majumbani zinazo oza na kufanya taka hizo kutumika kama mbolea inayoimarisha hali ya udongo kwa kutoa vimelea vyenye manufaa kama vile vitamini, asidi na madini ambayo yanatumiwa na mimea. Pia EM.1® hutumika kwenye mifugo kwa kuboresha vyakula na afya ya wanyama wafugwao.

KILIMO

Utengenezaji wa Mbolea ya Mboji

Changanya EM.1® na maji kwa kipimo cha lita moja ya EM.1® na Lita 50 za maji (1:50) au Mls 400 kwa Lita 20 za maji. Nyunyiza mchanganyiko huo kwenye mkusanyiko wa taka za kutengeneza mbolea ya mboji kwa kila mpangilio wa taka. Mbolea itakuwa tayari na harufu nzuri ya udongo baada ya muda wa kama mwezi mmoja. EM.1® inasaidia kuozesha mbolea ya mboji kwa haraka zaidi.

EM.1® pia inaweza kutumia kugeneneza bidhaa mbali mbali za kiasili kama viua wadudu kwa kutumia mimea ya asili inayojulikana kama EM.1® Fermented Plant Extract (EM.1® FPE). Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi.

MIFUGO

a). Kuku: Changanya Mls 5 za EM.1® kwa lita moja ya maji ya kunywa kila siku. Pia changanya 10mls ya EM.1® kwa kila kilo 5 ya chakula cha kuku. Wape kuku mchanganyiko huu. Mchanganyiko huu utaongeza uwezo wa kuku kusaga chakula na utaongeza vitamini ambazo zitamwezesha kuku kutaga mayai bora na kuwa na nyama nzuri isiyokuwa na harufu.

b). Mifugo Mingineyo  kama Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, Farasi, n.k.: Changanya Mls 50 za EM.1® kwenye lita 20 za maji ya kunywa na pia unaweza kunyunyuzia Mls 10 za EM.1® kwenye kilo 10 za chakula cha wanyama.

MAZINGIRA

a). Usafishaji wa Maji Taka

Mwaga katika kipimo cha 1:500 hadi 1:1,000 kwa kiasi cha majitaka mfululizo kwa muda ya siku tatu. EM.1® itasaidia kupunguza harufu mbaya na kusaidia kuozesha taka ngumu na kupunguza kiasi cha kemikali (B.O.D and C.O.D). Inaleta matokeo endelevu kama utarudia kumwaga lita moja ya EM.1® kwa kila lita 5,000 (1:5,000) kwa kila wiki.

b). Kupunguza Harufu Mbaya

Nyunyizia au Dondosha EM.1® iliyochanganywa na maji kwa kipimo cha 1:20 hadi 1:50. EM.1® itasaidia kupunguza harufu mbaya kwenye choo, zizi la mifugo na mahali pa kutupa takataka, kwenye mbolea ya mifugo na katika mabomba ya majitaka na sehemu nyingine zenye harufu inayotokana na uozo.

TAHADHARI

  1. Soma maelezo kabla ya kutumia bidhaa hii
  2. Weka mbali na watoto
  3. Inaweza kusababisha muwasho kwenye macho au ngozi. Osha kwa kutumia maji.
  4. Usiitumia kama chakula au dawa kwa binadamu.

Vimelea Vilivyomo

  • Baketria wa Mwanga –        Rhodopseoudomonas palustris
  • Bakteria wa Maziwa –        Lactobacillus plantarum and Lacobacillus casei
  • Hamira Saccharomyces cerevisae
  • Molasisi
  • Maji

MATUMIZI YA EM.1®

Weka Kwenye maji ya kunywa  kwa kipimo kifuatacho wape wanyama hawa

Kuku, Bata, kware, kanga, Ng’ombe, nguruwe, mbwa, Mbuzi, Sungura nk

Kipimo ni 10ml cha EM Ax  kwenye maji ya lita 5.Tumia kipimo 50ml kwa maji lita 10 kupulizia kwenye banda la Nguruwe na Ngo’mbe kwa ajili ya kuondoa harufu.Kama kunanuka sana tumia hadi 200ml kwa maji lita 10

Matumizi ya EM.1® kwenye kulisha wanyama

Changanya kilo moja ya Feedpro bokashi (kirutubisho cha EM) kwenye kilo 100 za chakula cha mnyama wako.

Matumizi ya EM.1® kwenye kuondoa harufu mbaya kwenye mabanda ya kuku

Tumia bidhaa ya EM.1® maalum kwa kumwaga mwaga kwenye banda kwa ajili ya kuondoa kabisa mazalia ya wadudu wabaya na harufu mbaya. (Feedpro Bokashi kwa Mazingira)

Kwa kuzibua choo kilichojaa

Weka EM.1® Safisha  kwenye chamber ya choo iliyojaa na bacteria hawa wa Em watakusaidia kula na kuondoa harufu ndani ya wiki chache tatizo litakuwa limeisha Pata bidhaa yetu ya lita tano kwa kuweka kwenye choo. Lita 10 zinatosha kwa chamber ya ujazo wa lita 1000.

Kwa kudekia eneo lenye mainzi wengi

Hakikisha umechanganya em na maji ya kudekia fanya usafi vizuri inzi watakimbia kama ni nje hakikisha unamwaga mwaga maji yenye EM.1®. Kipimo ni 50ml kwa maji lita 5.

Matumizi ya EM.1® kuzalisha funza kama chakula cha kuku

Weka EM.1® 5ml kwenye kikombe cha nusu lita tumia hayo maji kunyunyuzia kwenye ndoo ya uchafu wa jikoni ndoo au pipa liwe na matundu kuruhusu maji maji kupita, itaondoa harufu pia utapata funza waache wakue ni vizuri ukawa na ndoo mbili. Chukua funza wape kuku wa kienyeji hiyo ni protein ya asili.

EM.1® Kwenye Kilimo

Tumia 10ml kwenye maji lita 5 tumia kumwagilizia bustani.

Ni vizuri ukatumia mazo booster pamoja na mbolea za samadi wakati wa kuanzaa shamba. Kipimo ni 100gm kwa kila mita moja ya mraba.

Kwa matokeo mazuri hakikisha umeshaweka mbolea kwenye ardhi kabla ya kupanda mazao.

Umia EM.1® kwa 50ml na maji lita 10 kupulizia kwenye miti ya matunda kama miembe, michungwa , korosho etc kwa wiki mara moja hii inaongeza uwezo wa maua kutokuanguka

Faida za EM.1® na Matokea yaliyopatikana kutoka kwa wakulima wetu.

  • Kuondoa harufu mbaya kwenye nyumba za mifugo yao
  • Tumeweza kuondoa malalamiko ya majirani na kesi mbalimbali serikali za mtaa kwa kudhibiti harufu mbaya.
  • Uzalishaji kuongezeka na yenye ubora wa hali ya juu. Mfano utagaji kwa kuku, mayai yenye ubora makubwa , uwezo mkubwa wa mayai kutotolewa na ukuaji wa kasi kwa mifugo
  • Kusaidia tatizo la wanyama kuingia heat kwa wanyama kama ng’ombe na nguruwe
  • Uzalishaji wa maziwa upo ushuhuda wa kuongezeka kutoka lita 4 kwa siku hadi lita 8 kwa siku ndani ya wiki mbili tu za kutumia EM.1® ten ubora wa hali ya juu.
  • Kudhibiti magojwa ya mara kwa mara kwa mifugo.
  • Nyama kuwa tamu na isiyo na harufu au shombo.

Muda wa matumizi na Uhifadhi

  1. Bidhaa hii inakuwa bora kwa mwaka mmoja kabla ya kufunguliwa
  2. Funika Chupa ya EM.1® vizuri kila wakati umalizapo matumizi. Ihifadhi chumbani au kwenye sehemu isiyokuwa na mwanga wa moja kwa mmoja wa jua.
  3. Usiitumie kama utasikia harufu mbaya kwenye chupa
JINA LA BIDHAA MATUMIZI YAKE KIPIMO MAELEZO
EM.1® (LITA MOJA) Kwa wanayama kunywa kwenye maji yao.

Kwa umwagiliaji shambani baada ya kupanda mazao

Kwa kupulizia kwenye mazao yao pamoja na mazao ya miti kama maembe , michungwa.

Kupuliza kwenye ngozi za mifugo yako kana ng’ombe, nguruwe, mbuzi etc.

Tumia 40ml kwa maji lita 20. Utahitaji :

EM.1® lita moja

Molases lita 1

Maji lita 18.changanya vizuri funika vizuri mfuniko ukaze hifadhi kwa siku 7.

FEEDPRO BOKASHI (KILO MOJA) NA KILO 40 Changanya kwenye chakula cha mnyama wako mpe chakula Tumia kilo moja ya bokashi kwa kilo 100 za chakula cha mnyama wako. Hifadhi eneo lililo na kivuli.

 

FEEDPRO MAZINGIRA (750 GM) Kuondoa harufu kwenye nyumba za mifugo ambao hawahitaji majimaji au katika mikoa ya baridi.

Kuweka kwenye taka za jikoni kuondoa harufu mbaya.

Tumia 50gm kwa eneo la mita moja ya mraba utarudia matumizi kutokana na hali ya mazingira ilivyo,
EMAX BIO LIQUID (500ML) Kwa wanayama kunywa kwenye maji yao.

Kwa umwagiliaji shambani baada ya kupanda mazao

Kwa kupulizia kwenye mazao yao pamoja na mazao ya miti kama maembe , michungwa.

Kupuliza kwenye ngozi za mifugo yako kana ng’ombe, nguruwe, mbuzi etc.m

Tumia 40ml kwa maji lita 20.
EMAX BIO PEST**** Kwa kupulizia shambani kufukuza wadudu waharibifu

Kwa mifugo kunywa kuongeza kinga dhidi ya magonjwa

50ml kwa maji lita 5