FeedPro Products

FEEDPRO EMAX > FeedPro Products

Feedpro Bokashi

Hii ni bidhaa inayotokana na EM.1® ambao husaidia kuongeza ulishaji wa wanyama kwenye vyakula vya mifugo kama vile kuku, bata, mbuzi, kondoo, farasi, ng’ombe, nguruwe, nk.

Faida zake: Kusaidia kukinga mifugo kutokana na magonjwa ya kuambukiza na kuongeza ukuaji— utagaji kwa kuku wa mayai maziwa kwa ng’ombe na mbuzi.

Matumizi: Tumia nusu kilo ya mchanganyio huu kwenye kilo 50 za chakula cha wanyama.

Kuhifadhi: Weka Mchanganyiko huu kwenye sehemu isiyokuwa na mwanga wa jua.

Vilivyomo: Pumba Mahindi, Mlonge, Maji, Molasses, EM.1®

Feedpro Mazao Booster

Hii ni bidhaa inayotokana na EM.1® ambayo ni kichocheo cha mbolea asili ya wanyama kama vile ng’ombe, kuku, mbuzi, nguruwe, nk. Pia mboji ya mashambani

Faida zake: Kusaidia kuchochea vimelea muhimu kwenye udongo ambavyo husaidia ukuaji wa mimea na kukinga magonjwa kwenye mimea na mazao mbali mbali.

Matumizi: Tumia nusu kilo ya mchanganyio huu kwenye eneo la mraba la mita 3 ambalo tayari lina mbolea ya wanyama au mboji

Kuhifadhi: Weka Mchanganyiko huu kwenye sehemu isiyokuwa na mwanga wa jua.

Vilivyomo: Pumba ya mazao, Maji, Molasses, EM.1®

Feedpro – Mazingira

Hii ni bidhaa inayotokana na EM.1® ambao husaidia kuondoa harufu mbaya kwenye mabanda ya kuku, bata, mbuzi, kondoo, farasi, ng’ombe, mbwa, kware, nguruwe, nk.

Faida zake: Kuondoa kabisa harufu mbaya kwenye mabanda. Kuuwa wadudu wanaosababisha magonjwa walioopo kwenye malalio ya wanyama.

Matumizi: Weka kiasi cha Gms 50 kwenye eneo la mita moja ya mraba kila baada ya siku tatu. Harufu ikiisha rudia kila baada ya wiki mbili. Kila ukifagia mbolea weka baada ya kufagia.

Vilivyomo: Maranda yaliyosagwa,Maji, EM.1®, Molasses